Burudani

Chege aeleza kwanini anaonekana yeye na Temba ndani ya Kundi la TMK Wanaume Family

Staa wa muziki Chege Chigunda amesema Kundi la TMK Wanaume Family bado lina wasanii wake 7 ila kwa sasa mfumo wa biashara ya muziki umebadilika ndio maana mara nyingi hawatoi kazi za kundi zima.
Chege na Temba

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video ya wimbo ‘Sweety Sweety’ amekiambia kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa, yeye na Temba ni wasanii ambao tayari wameteneza ‘chemistry’ ambayo mara kwa mara mashabiki wamekuwa wakiihitaji.

“Wakati ule tunafanya nyimbo za kundi watu 7 au 8, muziki ulikuja ukachange, mashabiki wakawa wanahitaji sauti ya Chege na Temba peke yake,” alisema Chege.

“Tukajaribu kufanya ngoma moja inaitwa ‘Twenzetu’, tulifanya mimi, Temba na marehemu ‘YP’ pamoja na Ferooz ikapendwa sana, ndio ngoma ambayo ilinitambulisha mimi. Baada ya kutoa hiyo ngoma mimi nikatoa albamu yangu ambayo ndani yake kulikuwa na hiyo ngoma, wakati huo bado tunauza albamu kwa mhindi ‘Mamu’. Mamu akamwambia Fella mimi namtaka Chege na Temba, sisi tukaingia studio tukaanda albamu ya ‘Mkono Mmoja’, ikafanya vizuri sana. Sasa baada ya kufanya Mkono Mmoja na ikafanya vizuri sana mashabiki wakahisi sisi tumetoka Wanaume, lakini haikuwa hivyo,” alisema Chege.

Aliongeza, ‘Ili kuonyesha kundi lipo tukatoa ‘Kichwa Kinauma’, ikapendwa lakini bado watu wakamtaka Chege na Temba. Tukatoa ngoma mbili tatu ili kuweka sawa hiyo hali lakini bado. Sasa hivi kila mtu anametoa project zake binafsi, mimi nimetoa ‘Sweety Sweety’ na Temba katoa ‘Fundi’. Tunaangalia upepo unakujaje baada ya hizi kazi. Sema mashabiki wanakuwa hawajui mchezo nyuma ya pazia, wanakuwa wana tafsiri vingine mbona Chege na Temba ndio wanaonekana, lakini sisi tunacheza mchezo wetu kwa jinsi tunavyojua,”

Pia Chege alisema Kundi la TMK Wanaume Family bado lipo na lina wasanii wote 7.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents