Burudani

Couple 10 za mastaa waburudishaji zenye nguvu zaidi Tanzania – 2016

Tanzania imebarikiwa kuwa na tasnia ya burudani yenye watu wenye nguvu sana. Lakini nguvu yao huwa maradufu pale wakiwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa wenzao. Ninakuletea orodha ya couple 10 za mastaa wa Tanzania zenye nguvu zaidi kwa sasa. Nguvu zao zipo kwenye lundo la mashabiki walionao, ushawishi wao, utajiri wao na wafuasi walionao kwenye mitandao ya kijamii. Wengi ni kutokana na jinsi walivyodumu kwa muda mrefu, kutumia brand zao kwa pamoja kujikuza na mambo mengine kibao.


1. Diamond Platnumz na Zari the Bosslady

13395089_214032905662116_1444251759_n

Himaya ya Diamond yenye utajiri unaokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni 8 ina nguvu isiyoelezeka pale inapoungana na mwanamke aliyeachiwa utajiri mkubwa na ex wake na kujitengenezea himaya yake mwenyewe pia. Wanakaribia kufikisha miaka miwili sasa tangu wawe pamoja na ukikumbuka walivyoanza kwa kujiita ‘project’ hakuna aliyewahi kudhani kama wangeendelea kudunda hadi leo.

Sasa hivi ni wazazi wa mtoto wao mwenye miezi 11, Tiffah. Hii ni couple inayozungumzwa zaidi Afrika Mashariki, isiyokauka kwenye vichwa vya habari vya magazeti ya udaku kila iitwapo leo. Ni couple inayojadiliwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii na lundo la wafuasi walio nyuma yao tayari kwa kumshambulia yeyote anaye hatarisha uwepo wake, linatisha. Kwa pamoja wana wafuasi kwenye Instagram zaidi ya milioni 4.2 huku mtoto wao akiwaongezea wengine 700k na kuwa na takriban milioni 5.

Pamoja na hivyo, hii ni couple isiyokaukiwa misukosuko na skendo kibao zikiwemo za Diamond kuwahi kudaiwa kuchepuka na mrembo wa video ya Kwetu ya Raymond hadi tetesi kuwa Zari hana maelewano mazuri na ndugu za mchumba wake. Zari pia amekuwa akiwekwa kitimoto kwa kuendelea kuwa na mawasiliano na ex wake, Ivan, kitu ambacho hakiepukiki sababu wana watoto watatu wa kiume waliozaa pamoja.

Pamoja na hivyo, bado wameendelea kuonesha kutoteteleka na dhoruba hizo na mashua yao inaendelea kukata mawimbi baharini na huenda Tiffah akaja kupata mdogo wake, huku pia uwezekano wa kufunga pingu za maisha siku za usoni ukiendelea kuwa mkubwa.


2. Idris Sultan na Wema Sepetu

Wema

Mshindi wa Big Brother Africa aliyegeuka kuwa milionea ndani ya miezi mitatu na Miss Tanzania 2006 na muigizaji maarufu zaidi wa filamu Bongo wanapounda umoja wa kimahaba, matokeo yake ni makubwa. Idris Sultan na Wema Sepetu wana nguvu kubwa ambayo couple pekee iliyo na cheche za kuwazidi ni hiyo ya juu.

Hata hivyo yote yanarudi na kuanzia nyuma tena. Wema alikuwa kwenye uhusiano maarufu na wa muda mrefu na Diamond ambao bahati mbaya pamoja na kuachana, hadi leo harufu za mahaba yao zimeendelea kuwanyemelea na kutengeneza chuki na upendo kwa pamoja.

Idris alijikuta akizidiwa na nguvu ya umaarufu wa uhusiano wao hadi kuapa kutouweka hadharani tena – kitu ambacho kinaonesha ni kigumu kukifanikisha. Wao pia walikaribia kufika kwenye hatua muhimu ya kupata mtoto – mapacha, lakini kwa maneno yao wenyewe, Mungu hakupenda iwe hivyo. Bado suala la Wema kutopata mtoto limeendelea kuwa kidonda kibichi kinachotoneshwa mara nyingi.

Idris na Wema wamepitia majaribu mengi ambayo wakati mwingine huyashindwa kuyahimili na kuachana, lakini hugundua bado wanapendana na kurudiana tena. Kwa mfano kipindi video ya Wema imesambaa mtandaoni akimbusu mwanaume mwingine, iliuvunja moyo wa Idris kiasi cha kuamua kulivua pendo – kwa muda.

Hivi karibuni pia baada ya Wema na Diamond kuonesha kuvunja uhasama wao, Wema kumtumia salamu za siku ya kuzaliwa Bi. Sandra (mama yake Diamond) Idris alitafsiriwa na wengi kujikuta njia panda kwa mtazamo kuwa hapewi heshima anayostahili na mpenziwe. Hata hivyo hakujali na kwa wale waliohudhuria show yao ya Black and Tie, mwishoni mwa wiki, walishuhudia jinsi njia hao walivyokuwa wakitembea kama kumbi kumbi – mapenzi tele.

3. Alikiba na Jokate Mwegelo

KIba

Pamoja na wao wenyewe kuendelea kukwepa kukiri hadharani kuwa ni mtu na mpenzi wake, ni kipofu pekee asiyeweza kutambua pendo zito lilivyowajaa, Alikiba na Jokate Mwegelo. Wamekuwa pamoja kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kiasi ambacho uhusiano wao sio siri tena katika familia za pande zote mbili – ikiwa ni pamoja na Jokate kutambua na kujali uwepo wa watoto wa Alikiba.
Wamekuwa wakitengeneza headlines nyingi mno kwenye magazeti ya udaku kuhusu uhusiano wao lakini hadi sasa hawataki kuwapa kile mashabiki wao wamekuwa wakikiota kwa muda mrefu – kuuweka uhusiano wao wazi kama couple hizo juu.

Kitendo cha kuficha mahusiano yao si kigeni hata katika maisha yao ya nyuma. Pamoja na kuwahi kuwa na uhusiano na Hasheem Thabeet na kisha Diamond kwa muda mfupi, Jokate hajawahi kupendelea kuweka wazi maisha yake binafsi.

Alikiba pia vivyo hivyo, pamoja na kuwa na watoto watatu hadi sasa, kila mmoja na mama yake, hakuwahi kuwa mtu wa kuwaweka wazi wapenzi wake. Vyovyote ilivyo, mapenzi yao yanaonekana wazi kwa wale waliowahi kubahatika kuwaona wakiwa pamoja na pengine kuna siku wataamua kuuweka rasmi uhusiano wao kama mastaa wengine.

4. Jux na Vanessa Mdee

Jux and Vanessa Mdee

Iliwachukua muda mrefu sana Jux na Vanessa Mdee kukiri kuwa ni wapenzi. In fact, pamoja na kuamua kuuweka wazi, bado si watu wanaofurahia sana mada ya uhusiano wao. Wana takriban miaka miwili sasa tangu waanze kuwa pamoja.
Kuna wakati waliamua kuuweka wazi kidogo uhusiano wao kwa kuweka picha zao wakiwa kwenye mitandao ya kijamii, lakini sasa wameamua kuacha japo kwa walio karibu nao wanafamu jinsi wawili hawa wanavyopendana na kusaidiana katika kazi zao.

Kuna wakati pia Jux alimtumia Vee kwenye video yake lakini pia mara kibao Jux amekuwa karibu na mpenzi wake wakati akishoot video zake SA – mfano wakati akishoot video ya Never Ever.

Nina uhakika kuwa Jux ana ushindani mkubwa kuhakikisha kuwa Vee anaendelea kuwa wake daima na hii ni kutokana na umaarufu alionao Vanessa barani kote huku safari za nje zikiwa hazikauki. Jux pia kwa upande wake anafahamika kwa maisha ya kifahari aliyonayo na hivyo kujitengenezea sumaku inayovutia warembo wengi, achilia mbali maisha yake ya kusafiri mara kwa mara kwenda China masomoni.

Kwa namna yoyote ile, wawili hawa wanaonekana kuendana vyema na nina uhakika bado wana miaka mingi ya kuendelea kuwa pamoja.

5. Master J na Shaa

Master-J

Master J na Shaa walikutana takriban miaka kumi iliyopita. Shaa alikuwa msichana mdogo ambaye damu ya kufanya muziki ilikuwa ikichemka na kushinda shindano la Cocacola Popstars. Master J aliteuliwa kwenda nao Afrika Kusini kama producer wa kundi lililoanzishwa, Wakilisha. Baada ya kurudi, Shaa kwenda tena Marekani kusoma na kundi likavunjika, Shaa alirejea na kuwa chini ya MJ Records.

Sifahamu uhusiano wao kimapenzi ulianza lini lakini wana muda mrefu sana kwa sasa. Uhusiano wao umepitia majaribu mengi pia kuanzia Master J kutengana na mke wake aliyezaa naye watoto watatu warembo wa kike hadi Shaa kulalamikiwa kuwa sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo. Master J amewahi kukiri mara nyingi kuwa kuvunjika kwa ndoa yake lilikuwa jaribu kubwa zaidi katika maisha yake. Hata hivyo yeye na Shaa waliendelea kuwa madhubuti na hivi karibuni walidai kuwa wana mpango wa hatimaye kufunga ndoa.


6. Barakah Da Prince na Naj

13628138_1240767765933440_485090523_n

Kupanda chati na kufahamika haraka kwa Barakah Da Prince hakujatokana na hits zake tatu pekee – Siachani Nawe, Nivumilie na Siwezi, bali jinsi anavyoitupa karata yake kwenye masuala yahusishayo moyo. Amewahi kuhusishwa kuwa na uhusiano na list ndefu ya mastaa wakiwemo Meninah, Linah, Agnes Masogange, Nisha na hatimaye sasa akiwa na Naj aliyemrasimisha zaidi.

Naj, historia yake yake naye ni ya kipekee. Hakupata jina kupitia hit single yake na Mr Blue ‘Please Don’t Go’ tu bali kwakuwa na uhusiano na rapper huyo aliyemtumia pia kwenye video ya hit single yake, Tabasamu.

Barakah amekuwa mpenzi wake wa kwanza tangu aliporejea kutoka Uingereza alikokuwa masomoni kwa miaka mingi. Kwa sasa penzi la msanii huyo mpya wa Rockstar4000 na Naj limezidi kupamba moto na hawaoni haya kueleza wazi wanavyopendana.

7. Majizzo na Lulu

13557244_171259513288748_1474298025_n

Nilianza kuona dalili za kuwepo uhusiano wa Majizzo na Lulu miezi kadhaa iliyopita wakati wa tuzo za Africa Magic jijini Lagos. Majizzo alimsindikiza muigizaji huyo ambaye jina lake halisi ni Elizabeth Michael na akawa bahati kwake kwasababu alishinda.

Baada ya hapo tetesi za uhusiano wao zikawa kubwa zaidi. Uhusiano wao sasa unaonekana kuwa wazi zaidi licha ya kuzungukwa na maneno ya hapa na pale hasa kutokana na Majizzo kuachana na mzazi mwenzake, Hamisa Mobetto. Warembo hao kwa sasa ni kama paka na panya na timu zao zimewahi kurushiana vijembe mtandaoni.

Bado hata hivyo Majizzo na Lulu hawajataka kuyaweka wazi mambo ya faragha mara kwa mara na hivyo kuwafanya wengi kutaka kuwachimba zaidi.

Umaarufu na ushawishi wa Lulu ukiunganishwa na sifa za ujasiriamali na utajiri alionao Majizzo (Dj maarufu aliyewika zamani) kwakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EFM unaifanya couple hii iwe na nguvu sana.

8. Harmonize na Jacqueline Wolper

e0ca9c67-c1e2-49d5-8fad-aef387a7d3b9

Harmonize ametoka kwenye maisha duni ya kulala stendi ya mabasi hadi kusaini label inayomilikiwa na msanii mkubwa Afrika. Hiyo haikutosha, alienda mbali zaidi kwa kuanzisha uhusiano na mmoja wa mastaa wakubwa wa filamu nchini na gwiji wa fashion, Jacqueline Wolper.

Hadithi ya uhusiano wao inavutia pia. Wolper aliwahi kuwa na uhusiano na Diamond ambaye leo hii wamebaki wakiitana ‘mkwe’ huku Harmonize akipewa baraka za kufaidi kilichowahi kuwa mali ya bosi wake. Uhusiano wao uliteka vichwa vya habari ndani ya muda mfupi. Wengi walidhani ni kiki lakini baada ya muda mfupi kila mmoja alishangaa jinsi walivyozama kwenye mahaba mazito.


9. Quick Rocka na Kajala

Kajala-na-Quick

Nimeanza kuusikia uhusiano wa Quick Rocka na Kajala muda mrefu sana. Wao pia hawakuwa tayari kuuweka wazi na waliendelea kukanusha kuwa pamoja kwa kipindi kirefu. Lakini kama wasemavyo kuwa penzi ni kikohozi kulificha huwezi uhusiano wao ulithibitishwa katika mazingira tofauti tofauti ikiwemo video aliyopost Quick akimbusu muigizaji huyo.

10. Nahreel na Aika

12543287_1125680584111594_2090272718_n

Nahreel na Aika wametoka mbali. Kutoka kusoma pamoja India wakiwa na kundi la Pah One, hadi kutengeneza si tu kundi maarufu Afrika Mashariki, Navy Kenzo bali pia kuanzisha studio na label yao, The Industry. Kwa wanaowafahamu, watakubaliana nami kuwa, Nahreel na Aika si tu wapenzi, bali pia ni mtu na mshkaji wake na partiners kibiashara wanaoelewana kinoma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents