Burudani

Cyril amuunga mkono ‘Yeezy’ aliyempa kichapo paparazzi, ‘badomimi kudunda mtu’

Kanye West ana mtu wa kumtetea kwa kitendo alichokifanya juzi kwenye uwanja wa ndege wa LAX nchini Marekani. Rapper mwenye asili ya mkoani Singida, Cyril aka Kamikaze, amemuunga mkono Yeezy aliyeamua kumfundisha adabu mmoja wa mapaparazzi waliokuwa wamejaa kwenye uwanja huo wa ndege kumpiga picha.

kanye-paparazzo-1

“Tunatokea mtaani ,tunajua jinsi yakua wahuni vile vile..majina u fame usikudanganye …jichanganye uoneshwe michezo.. #ganstarganstar #kanyewest katisha pu*bav zao maswala ya kuingiliana private life sio issue..#badomimi #kudundamtu, “ameandika Cyril kwenye Instagram.

Hata hivyo, Kanye West sasa hivi anakabiliwa na kosa la jaribio la unyang’anyi baada ya kujaribu kumnyakua paparazzi huyo aitwaye Danio camera yake alipokuwa akiwasili kwenye uwanja huo wa ndege siku ya Ijumaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents