Habari

Family Reunion: Baada ya kutokuwa na maelewano tangu akiwa na miaka 7, Shetta na baba yake mzazi wapatana

Baraka za mwezi Mtukufu wa Ramadhan, zimeitembelea familia ya Baba Qayllah, Shetta Bilal. Baada ya miaka mingi ya maelewano hafifu na baba yake mzazi, leo baba na mwanae wameamua ‘kuLizika shoka’ (bury the hatchet) na kuanza ukurasa mpya.

4a3b911cf20f11e2aa5e22000aa80116_7

Kupitia Instagram, Shetta amepost picha (hiyo juu) akiwa na baba yake mzazi Mzee Bilal ambaye ni Sheikh, pamoja na mdogo wake Awab na kuandika: Wit my daddy n my young broda Awab….. #happyday baada ya miaka mingi kuwa na tofauti na mzee tangu nina miaka 7 leo yameisha #bassawa #Ramadankareem.”

Bongo5 imezungumza kwa simu na Shetta kutaka kupata maelezo zaidi ya kwanini alikuwa haelewani na baba yake.

“Basi tu tulikuwa tunakosana, nahisi situations zangu na maisha yangu vilikuwa haviko sawa. Kazi yangu ninayofanya na nini kwasababu yeye ni mtu wa dini sana, baba yangu ni Al Haj, Sheikh. Kwahiyo nahisi hilo lilikuwa tatizo kwa upande wake..”

Shetta amesema kwa muda wote huo baba yake alikuwa hamfahamu mke wake pamoja mwanae, Qayllah lakini sasa anafuraha kwakuwa wameyamaliza bab yake amemuelewa.

Msikilize zaidi hapa:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents