Burudani

Cyrill atoa jina la Raymond kwenye wimbo wake mpya

Cyrill Kamikaze ametoa jina la Raymond kwenye wimbo wake mpya ‘Cheza Kidogo’ baada ya uongozi wa WCB kuukana.

Cyrill

Siku ya Jumanne, Cyrill aliachia wimbo wake mpya na kusema kuwa amemshirikisha msanii kutoka lebo ya WCB, Raymond lakini kupitia akaunti yake ya Twitter, meneja wa Diamond, Sallam Sharaff aliandika: “Hakuna Collabo na Raymond, alimuomba Ray amuandikie na apewe melody siku nyingi sana! Hiyo nyimbo hatuuitambui.”

Kutokana na taarifa hizo zilizoanza kuchanganya vichwa vya mashabiki, Cyrill kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika:

“Ok nadhani issue ilikuwa ni kumtaja Ray kuwa nimemshirikisha na kiukweli ameshiriki kuandika huu wimbo asilimia 70 nzima na hata kuweka sauti zake na deal tukaikamilisha na kazi tumeifanya kabla Ray hajaenda label mpya kama nilivyo sema jana .. Basi jina nimelitoa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents