Videos

Daraja Walk: Rapper HHP wa Afrika Kusini aja Tanzania kwa miguu kuhimiza umoja wa Afrika

Rapper wa Afrika Kusini, Jabulani Tsambo aka HHP yupo nchini Tanzania ambapo amekuja katika muendelezo wa safari yake kwa miguu kutembea katika nchi mbalimbali barani Afrika kupromote umoja na mshikamano.

HHP ameipa safari yake jina ‘Daraja Walk’ (daraja Kiswahili, bridge) na itachukua zaidi ya miezi sita kutembea umbali wa kilomita 6,000.

“I refer to my journey as Daraja, which means ‘bridge’ in Swahili. I want to build a bridge and unite African countries as I travel through them,” alisema HHP kuelezea madhumuni ya safari hiyo.

Katika safari yake, HHP akiwa na washkaji zake akiwemo DJ Zondi, watakuwa wakifanya majadiliano kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu vijana wa Afrika. Huko hukutana hufanya mahojiano kwenye vyombo mbalimbali vya habari na collabo za hapa na pale na wasanii wa nchi husika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents