Habari

Utafiti: Unywaji wa kahawa zaidi ya vikombe 4 kwa siku unaongeza hatari ya kufa katika umri mdogo

Utafiti unaonesha kwamba unywaji wa zaidi ya vikombe 4 vya kahawa kwa siku unaweza kuchangia hatari ya uwezekano wa vijana wenye umri mdogo kufa mapema, lakini hii ni kwa wale wa chini ya miaka 55.

coffe cup-1

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa Marekani unywaji wa vikombe 28 kwa wiki unaongeza uwezekano wa vifo vya mapema kwa vijana. Utafiti huo uliofanywa kwa maisha ya watu wa Marekani ulihusisha watu 43,727 wa kuanzia miaka 20 hadi 87.

Mtafiti Steven Blair, wa University of South Carolina, Marekani amesema matumizi ya kahawa kwa wingi yanaweza kusababisha athari katika mwili na watu wenye ‘coffee addiction’ ndio wako katika hatari kubwa zaidi.

Hata hivyo watafiti hao hawakueleza sababu za kwanini kahawa haijaonekana kuwa na madhara kwa watu wa zaidi ya miaka 55 kama utafiti walivyoonesha kwa vijana. Kahawa ina kemikali nyingi tofauti ambazo zinaweza kuwa na athari na faida pia kwa afya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents