Burudani

Darassa aongeza nguvu ya Mr Blue kwenye ngoma mpya

Rapper Darassa ameamua kutoitoa ngoma yake ‘No retreat No surrender’ aliyokuwa amepanga kuitoa na badala yake ataachia wimbo aliomshirikisha Mr Blue.

1597135_1593644797548150_1828612772_n

Darassa ameiambia Bongo5 kuwa amepokea ushauri wa kufanya hivyo kutoka kwa uongozi wake.

“Kazi yangu ambayo ilikuwa inakuja ni ‘No retreat No surrender’ na tayari ipo fresh, lakini kutokana na watu wangu wa karibu pamoja na uongozi wangu kunishauri, ninaweza kuitoa baadaye sana na sasa nitaendelea kutoa nyimbo nyingine kwa sababu sasa hivi bado nipo kwenye harakati,” amesema.

“Baada ya kukubaliana hivyo nikaona hii ni nafasi ya kuachia kazi zangu nyingine, kwahiyo sasa hivi kuna kazi nimefanya na Mr Blue hii ndio itaanza kutoka. Pia nimefanya kolabo na Rich Mavoko na zote zipo kwenye kiwango kizuri,” ameongeza.

Darassa amesema huu ni muda wa kuanza kutoa kazi alizofanya na wasanii wengine na kwamba wimbo aliomshirikisha Mr Blue umetayarishwa na Mr Touch na utatoka baada ya mwezi wa Ramadhan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents