Burudani

Davido ndiye aliyeniita, kupiga Kwa Ngwaru nikaona nisije nikaharibu show ya watu – Diamond (+video)

Msanii wa Bongo Flava, Diamond amefunguka kuhusu ishu ya kuibuka ghafla katika show ya msanii kutokea nchini Nigeria, Davido.

Muimbaji huyo akizungumza leo June 19, 2018 na waandishi wa habari Dar es Salaam, amesema kuwa Davido ndiye aliyemtafuta kupitia mtandao wa Instagram na yeye akaliwasilisha kwa uongozi wake ambapo waliliridhia.

“Basi nilipofika pale watu walinipokea kwa nguvu kubwa sana, kesho yake habari ikawa ni hiyo tu. Nikapiga Kwa Ngwaru kidogo tu nikaisimamisha nikaona nisije nikaharibu show ya watu,” amesema Diamond.

Show ya Davido ambayo ilifanyika Next Door weekend iliyomalizika ilipambwa na wasanii wengine kutoka Bongo kama Ruby, Nandy na The Mafik.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents