Burudani

DeeAndy: Uhusiano wangu na Godzilla una miaka 2 sasa

Hawakuwahi kusema hadharani kuhusu uhusiano wao wa kimapenzi, lakini wengi walikuwa wakiona ukaribu wa kimahaba uliopo kati ya rapper wa ‘Sala Sala’ Godzilla na mtangazaji wa Clouds FM, DeeAndy.

10655142_699622523460531_1121467933_n

Mtangazaji huyo wa 255 ambayo ni sehemu ya kipindi cha XXL, amelazimika kuthibitisha uhusiano wake na rapper huyo anayesherehekea siku yake ya kuzaliwa Jumatatu hii baada ya watangazaji wenzie, B12 na DJ Fetty kumbana.

Dee alidai kuwa uhusiano wao kwa sasa umefikisha umri wa miaka miwili. “I think ilikuwa studio,” DeeAndy alijibu baada ya Fetty kumuuliza ni wapi walikutana na Zizi.

“Ilikuwa Tongwe,” alisema mtangazaji huyo na kuongeza kuwa alienda kufanya tangazo.

Kabla ya hapo pia, mrembo huyo aliandika ujumbe mrefu kwenye Instagram kumpongeza mpenzi wake huyo kwenye siku yake ya kuzaliwa.

“I could give you a thousand tokens and hundreds of gifts on your birthday today. but that means nothing until I give you the first and foremost unconditional love I receive from you on a daily basis… happy birthday to the man who brings out the best in me, the most selfless, loving, generous and hardworking man you’ll ever know, my rock, my right hand, but most of all, my best friend,” ameandika.

“We don’t only share time but a spiritual, mental and unique connection that cannot be broken! I thank God every night that he blessed me with a partner sooo loving , supportive , motivated , wise and sexy. I hope all your wishes and blessings not only come today on your birthday but throughout life and this year ! I love you down to every living molecule in your body ❤
Happy birthday @kingzilla_tz.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents