Habari

Young Tuso amchana Nikki Mbishi, asema ‘amesanda’ kimuziki

Rapper mchanga, Young Tuso amemchana Nikki Mbishi aka Dr Unju, kwa kudai kuwa msanii huyo ameshindwa kuhimili kasi ya rappers wapya na ndio maana ametangaza kuacha kufanya muziki.

01

Tuso amemchana rapper huyo kupitia 255 ya XXL ndani ya Clouds FM, Jumatatu hii. Pamoja na kumchana, Tuso amekiri kuwa hip hop bado inamuhitaji Nikki.

“Hizi habari kwanza zimenisitua lakini naona pengine muziki wa Hip Hop ulikuwa unamhitaji bado,” amesema Tuso. “Sijajua kwanini ameamua kuacha muziki, sijajua kwa kweli. Yeye kama yeye ni msanii mkali ambaye anajiamini, hakutakiwa kusema hivyo. Hivyo ni kusanda tu kwenye huu muziki,” ameongeza.

“Unajua naweza nikasema ameacha kwenye huu muziki akiwa anazungumzia sababu fulani kumbe inawezekana ni kusanda tu, kwamba Young mcees wanakuja vizuri si wadogo, wanaendelea kuchachafya. Labda anaona siku zinaenda halafu watu wanazidi tu kufanya mangoma, kwahiyo namhesabu kama MC aliyesanda. Kwanini aache kama yeye ni msanii mkali kabisa wa Hip Hop?, amehoji.

Tuso hakusita pia kufafanua maana ya ‘kusanda’.

“Kusanda ni kuchemsha kwenye jambo fulani, kushindwa, kwahiyo mimi nikisikia yeye ameacha muziki naona amechemsha kwenye rap game.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents