Habari

Defao azikwa kitaifa, hakuacha mtoto

Mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo François Lulendo Matumona, maarufu General Defao amezikwa jana siku ya Jumamosi katika mazishi ya kitaifa.

Defao alifariki mwezi Disemba mwaka jana katika hospitali Laquintinie huko Douala, Cameroon, ambako alikuwa akipokea matibabu.

Jamaa zake wanasema mwanamuziki huyu hakuacha mtoto lakini ameacha nyuma vito vya dhahabu vya thamani ya dola 260 za Kimarekani (mikufu ya dhahabu aliyokuwakuwa akivalia shingoni).

Wanamuziki wenzake na mashabiki wake waliohudhuri mazishi hayo wakiwa wamevalia mavazi za bei ghali wakidai pia Defao alikuwa mmoja wao, na wanafanya maonesho ya mavazi.

Related Articles

Back to top button