Burudani

Diamond: Wasafi Festival Dar naahidi tutaandika historia itakayoiweka Bongo Fleva kwenye kumbukumbu ya Dunia

Msanii wa muziki, Diamond Platnumz bado anaendelea kuandika historia kupitia Tamasha la Wasafi Festival baada ya wiki hii kufanya show ya nguvu huko Mombasa Kenya.

Disemba 31 muimbaji huyo anafunga mwaka na show ya Nairobi Kenya huku akiwaahidi Watanzania kwamba Wasafi Festival Dar es salaam itaandika historia itakayoiweka Bongo Fleva kwenye kumbukumbu ya Dunia.

Wasafi Festival Dar ilikuwa ifanyike kabla ya Nairobi na Mombasa lakini baada ya kuona tarehe zinaingiliana na matasha ya mengine ya Dar akaona aighailishe na afanye wakati mwingine ambao mpaka sasa bado hajauweka wazi.

“MOMBASA LOVE🌷….. COMORRO!!! am in Town…. i can’t wait to see you tomorrow…..NAIROBI!!! Let’s make another History on the 31st Dec…… DAR ES SALAAM!!!! Mwenyez Mungu akijaalia, Nawahidi kwa pamoja tutaandika Kumbukumbu ambayo itaiweka BONGOFLEVA yetu kwenye Kumbukumbu ya DUNIA🌍#WasafiFestiValKenya2018,” aliandika Diamond Instagram.

Show ya Mombasa inatarajiwa kuwakutanisha mastaa wa Tanzania, Kenya huku Marekani ikitarajiwa kuwakilishwa na Morgan Heritage.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents