Habari

Dkt Mpoki awaasa wafanyakazi kujiepusha na vitendo vya rushwa

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya amewahasa wafanyakazi wa Wizara hiyo kujiepusha na vitendo vya kupokea rushwa pindi watoapo huduma kwa wananchi.


Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Edward Mbanga akiwasilisha bajeti mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya katika kikao hicho

Akizungumza hayo wakati wa kikao cha uzinduzi wa baraza jipya la wafanyakazi wa wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto uliofanyika leo jijini Dar es salaam ambapo wajumbe wa baraza hilo walikutana kwa pamoja.


Wageni waalikwa na Wajumbe wa Baraza la Wafanya kazi wa Wizara ya Afya wakifuatilia kwa umakini mjadala uliokuwa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya katika kikaohicho

“Nitumie fursa hii kuwaasa watumishi wote kuacha kufanya kazi kwa mazoea ikiwa ni kujiepusha na vitendo vya rushwa,uzembe,majungu na ufisadi kwani kama mnavyojua sekta ya Afya ni miongoni mwa sekta zinazopigiwa kelele na wadau mbalimbali juu ya vitendo vya rushwa,” alisema Dkt. Mpoki.

Aidha Dkt. Mpoki alisema kuwa watumishi wanapaswa kukataa vitendo viovu sehemu zao za kazi na kupinga vitendo vya rushwa kwa hiari na kuhakikisha tuhuma hizo zinakwisha kwa kuchukua hatua madhubuti za kuboresha mifumo ya utendaji kazi.

Mbali na hayo Dkt. Mpoki amewasisitiza watumishi kupima afya zao mara kwa mara ili kujua mustakabari wa afya zao pamoja na kuwa na tabia ya kufanya mazoezi kwani wanatumia muda mwingi kukaa ofisini.

Kwa upande wake Mtoa mada kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi, Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Bi. Tulia Msemwa amesema kuwa kazi kubwa ya Baraza hilo la Wafanyakazi kuishauri Wizara kuweza kutoa huduma bora na sahihi kwa wananchi bila ubaguzi.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents