Burudani

Dogo Janja: Dar wananichukulia poa, nyimbo nyingi ntazifanyia Arusha

Dogo Janja amesema kwa sasa atakuwa anafanya nyimbo zake nyingi nyumbani kwao jijini Arusha kwakuwa watu wa Dar es Saalam wanamchukulia poa.

10177945_866628860030183_3359152225810379564_n

Rapper huyo Akizungumza na bongo5 leo Dogo Janja amedai kuwa nyumbani kwao Arusha anathaminiwa kuliko Dar Es Saalam.

“Endapo nikihitaji kufanya kazi na B’Hits nitafanya nao ila nimeplan asilimia ya ngoma zangu nyingi niwe nafanyia nyumbani kwasababu napata thamani kubwa sana kuliko ninayopata huko (Dar). Tatizo Dar watu wana mambo ya kuchuKUliana poa. Arusha kuna manufaa zaidi kwangu kuliko Dar. Sio kwamba sitafanya nyimbo Dar! Dar nitafanya nyimbo lakini sana sana official ngoma zangu nitazokuwa nafanya zitakuwa ni Arusha kwa asilimia nyingi. Mimi nakaa Dar na nafanya muziki wangu Dar ila ngoma zangu narekodia nyumbani unajua mwenye asili haachi asili na akiacha asili hana akili,” amesema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents