Habari

Donald Trump ampa shavu Ben Carson

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ameendelea na kazi ya kuteua viongozi kwenye nyadhifa tofauti tofauti ambao watashirikiana kuiongoza nchi hiyo.

ben-carson-heres-one-step-we-could-take-to-prevent-mass-shootings

Trump amemteuwa Dkt. Ben Carson ambaye alikuwa mpinzani wake kwenye uchaguzi wa ndani wa chama cha Republican kuwa waziri wa makazi na ustawi wa jamii.

Mpaka sasa Rais huyo ameshafanikiwa kuteuw viongozi kadhaa ambao watashirikiana kwenye safari yake hiyo ya uongozi akiwemo Reince Priebus, Stephen Bannon, Michael Flynn, Jeff Sessions na wengine.

Trump anatarajiwa kuapishwa Ijumaa ya Januari 20, mwakani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents