Bongo Movie

Dr. Cheni kumpa shavu Steve (shabiki wa Yanga) kwenye filamu yake ‘Nimekubali Kuolewa’

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Dr. Cheni amesema anatarajia kufanya filamu mpya iitwayo ‘Nimekubali Kuolewa’ atakayomshirikisha shabiki maarufu wa timu ya Yanga, Steve.

page

Akizungumza na Bongo5 jana, Dr.Cheni alisema Steve alimfuata kumuomba ampe shavu kwenye moja ya filamu zake kwakuwa anahisi ana kipaji cha kuigiza.

“Steve alinifata akaniambia anaweza kuigiza kwahiyo mimi nikajaribu kufanya naye mahojiano mafupi nikagundua anaweza baada ya kurejea kwenye tukio lake la kulia uwanjani. Nikaona nitafute wazo nifanye naye kitu ili imlipe ingawa aliniomba tu,” alisema Cheni.

“Nikatunga story ‘Nimekubali Kuolewa’ ambayo atakuwepo pia. Nitamilipa ingawa aliomba, ninajua kwa uwezo aliokuwanao nitamtengezea jina katika industry ya filamu nchini hivyo anaweza kupata issue nyingine akaweza kuendesha maisha yake vizuri.”

Dr Cheni alisema yeye ndiye aliweza kukiona kipaji cha Elizabeth Michael aka Lulu akiwa mdogo na kukikuza zaidi hadi leo amekuwa miongoni mwa waigizaji bora wa filamu Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents