Habari

Eddy Kenzo akutana uso kwa uso na Rais Museveni, Baada ya kuanza kampeni ya kuikosoa serikali mitandaoni

Msanii maarufu nchini Uganda, Eddy Kenzo amefanikiwa kuitwa Ikulu na kukutana na Rais wa taifa hilo, Yoweri Museveni kwa lengo la kupongezwa kwa kushinda tuzo ya AEA-USA nchini Marekani.

Wiki mbili zilizopita Eddy Kenzo aliiomba serikali ya taifa hilo, Imchukulie hatua kiongozi wa dini maarufu nchini humo, Sheikh Nuhu Muzaata, Kwa kosa la kumtukana mbele ya binti yake lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

Tukio hilo la Eddy Kenzo kutukanwa na Sheikh Nuhu Muzaata, Lilitokea wakati kiongozi huyo alipokuwa anafungisha ndoa ya aliyekuwa mke wa Eddy Kenzo, Mwanamuziki Rema Namakula.

Image

Sheikh kwenye harusi hiyo, Rema Namakula na mfanyabiashara mmoja aitwaye Hamzah, Alisikika akimpiga vijembe Eddy Kenzo kumuita mtu masikini, Malaya na asiyeweza kutunza mwanamke mzuri kama Rema.

Wakati anatoa kauli hizo kwenye tukio hilo, Rema alikuwa na mtoto wake wa kike ambaye amezaa na Ex wake Eddy Kenzo.

Image

Kauli hizo zilimfanya Eddy Kenzo atokwe na machozi na kuposti video mitandaoni akimtaka Sheikh huyo amuombe msamaha.

Eddy Kenzo alihoji pia kwanini? Sheikh huyo asichukuliwe hatua za kisheria ile hali wanaona anachafua jina lake kwa makusudi.

Mshindi huyo wa tuzo ya BET, Alianzisha hashtag ya #Weyayu? na watu wengi walimuunga mkono mitandaoni.

Baadhi ya wasanii wenzake kama Jose Chameleone alimtaka awe mvumilivu kwani ni mambo ya kupita na atalipwa na Mungu.

Watu wengi mitandaoni walitumia Hashtag hiyo kueleza namna serikali ilivyowasahau wasanii wa muziki nchini humo, Jambo ambalo linapelekea hata kukosa masuala mirahaba na kuibiwa kwa kazi za wasanii.

Wiki iliyopita wakati ameshinda tuzo hiyo ya Africa Entertainment Awards – USA kwenye kipengele cha “The African Entertainer of the year 2019, Aliuliza pia je, Serikali yake itampongeza au itaendelea kukaa kimya.

Rais Museveni ndiye alianza ku-tweet kwa kuandika “I met with recently crowned African Entertainer of the year and BET award winner, Edrisah Musuuza alias @eddykenzoficial. His story is one of resilience and hard work. Growing up as an orphan to a celebrated and inspirational artiste. I wish him and his team good luck.” .

Naye Eddy Kenzo, Aka-tweet na yeye kwa kuwashukuru watu wote waliounga mkono kampeni ya Weyayu, “HI GUYS !! THANK YOU THE HASHTAG WEYAYU I’M INVITED BY THE HEAD OF STATE. IN RECOGNITION OF MY CONTRIBUTION TO THE COUNTRY AND AFRICA AT LARGE. WHAT SHOULD I TELL HIM?“.

Na kisha akamshukuru Rais Museveni, “Thank you for your encouraging remarks. In response to my past post as I went to state house to meet the president. Indeed I want to confirm that I met him today in entebbe“.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents