Fahamu

Fahamu ugonjwa unaomsumbua Ommy Dimpoz, mtaalamu wa afya aeleza vyanzo vyake na kutoa tahadhari kwa wasanii (+Audio)

Huu ndio ugonjwa unaomsumbua Ommy Dimpoz, mtaalamu wa afya aeleza vyanzo vyake na kutoa tahadhali kwa wasanii (+Audio)

Ni mwezi sasa umepita tangu msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz atangaze hadharani kuwa afya yake haipo sawa baada ya kufanyiwa matibabu nchini Kenya bila mafanikio na kushauriwa kwenda nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

Ommy Dimpoz

Ingawaje Ommy Dimpoz hakuweka wazi ni ugonjwa gani hasa unaomsumbua lakini kwenye mahojiano yake na mchambuzi wa soka Tanzania, Eddo Kumwembe alinukuliwa akisema amefanyiwa upasuaji wa Koromeo.

Akielezea kwenye mahojiano hayo Ommy Dimpoz alisema kuwa  awali alianza kuona dalili za kukaukiwa koo na baadaye alishindwa kabisa kumeza chakula wala kitu chochote mdomoni.

Je,dalili hizo huenda zikawa za ugonjwa gani? Bongo5 tumemtafuta mtalaamu wa magonjwa ya kinywa na meno, Dkt. Onesmo Ezekiel Kapugi kutoka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (BOMBO) ambaye yeye ameleeza kuwa dalili hizo za kushindwa kumeza chakula kitaalamu inaitwa Dysphagia na ni dalili ya magonjwa ya vinywa.

Dkt. Kapugi amesema dalili hizo mara nyingi zinaweza kupelekea magomjwa ya Parkinson ambayo yanasababishwa na neva za fahamu kushindwa kufanya kazi vizuri ikiwemo kusinyaa kwa koromeo na hii huwatokea zaidi watu wenye umri mkubwa.

Akitaja chanzo hasa cha magonjwa kama hayo kwa wasanii amesema kuwa mara nyingi wasanii wanapoimba kwenye koromeo kuna kitu kinaitwa Vocal Cords na kama msanii ataimba kwa muda mrefu huwa vocal cords zinavimba na baadaye kupelekea maumivu kwenye koromeo na kushindwa kula wala kumeza kitu chochote.

Related image

Hata hivyo, Dkt. Kapugi amewasihi Watanzania kuwa na mazoea ya kupima afya zao au kwenda mara moja kwenye vituo vya afya pale wanapojihisi utofauti kwenye miili yao.

Sikiliza mahojiano ya Dkt. Kapugi na Bongo5 hapa chini:

 

Related Articles

10 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents