Fahamu

Fahamu: Viwanja 20 vya ndege vinavyotumika zaidi duniani.

Baraza la kimataifa la viwanja vya ndege limetoa orodha ya viwanja 20, vya ndege vilivyovunja rekodi ya kutoa huduma za safari za anga kwa mwaka 2016 tu.


Orodha ni hii hapa.

1.Atlanta -Marekani : Kilisafirisha jumla ya abiria 104,171,935 kwa safari za anga kwa mwaka 2016.

2.Beijing – China : Kilisafirisha jumla ya abiria wapatao 94,393,454 kwa safari za anga kwa mwaka 2016.

3.Dubai International (DXB)- Falme za Kiarabu: Kilisafirisha jumla ya abiria 83,654,250 kwa kipindi cha mwaka 2016 kwa safari za anga.

4.Los Angeles (LAX) Marekani – Jumla ya abiria 80,921,527 walisafiri kwa mwaka 2016.

5.Tokyo Haneda (HND) – Japan kilisafirisha jumla ya abiria 79,699,762 kwa safari za anga kwa mwaka 2016.

6.Chicago O’Hare (ORD) Marekani – Kilisafirisha jumla ya abiria 77,960,588 kwa kipindi cha mwaka 2016.

7.London Heathrow (LHR) Uingereza – Kilisafirisha jumla ya abiria wapatao 75,715,474 kwa mwaka 2016.

8.Hong Kong (HKG)-China Kilisafirisha jumla ya abiria wapatao 70,305,857 kwa safari za anga kwa mwka 2016.

9.Shanghai (PVG)- China : Kilisafirisha jumla ya abiria 66,002,414 kwa safari za anga kwa kipindi cha mwaka 2016.

10.Paris Charles de Gaulle (CDG)-Ufaransa : Abiria wapatao 65,933,145 walitumia usafiri wa anga kwa mwaka 2016.

11.Dallas/Fort Worth (DFW)-Marekani: Mwaka 2016 abiria 65,670,697 walitumia uwanja huo kwa safari za anga.

12.Amsterdam (AMS)-Uholanzi:– Abiria 63,625,534 walitumia uwanja huo kwa mwaka 2016 kwa safari za ndege.

13.Frankfurt (FRA)-Ujerumani – Ilitumika kusafirisha abiria wapatao 60,786,937 kwa mwaka 2016.

14.Istanbul (IST)-Uturuki :Jumla ya abiria 60,119,876 walisafari kwa kutumia ndege kwa mwaka 2016.

15.Guangzhou-China (CAN) – Abiria 59,732,147 walisafiri kwa kipindi cha mwaka 2016.

16.New York JFK (JFK)-Marekani – Abiria 58,873,386 walitumia usafiri wa anga kwa mwaka 2016.

17.Singapore (SIN) – Abiria 58,698,000 walisafiri kwa anga kipindi cha mwaka 2016.

18. Denver (DEN- Marekani – Jumla ya abiria 58,266,515 walisafiri kwa mwaka 2016.

19.Seoul Incheon (ICN)-Korea Kusini – Jumla ya abiria 57,849,814 walisafiri kipindi cha mwaka 2016 kwa usafiri wa anga.

20. Bangkok Suvarnabhumi (BKK)-Thailand – 55,892,428 walisafiri kwa kipindi cha mwaka 2016 kwa kutumia usafiri wa anga.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents