Habari

Femina Hip waja na shindano la ‘Ruka Juu’ kivingine (Video)

Shindano la vijana wajasiriamali kwenye runinga la Ruka Juu linaloandaliwa na Femina Hip limerudi upya ambapo litaanza kuonyeshwa kuanzia October 1 saa moja jioni katika kituo cha runinga cha EATV.

Kipindi hicho kitakuwa na wiki 12 za kujifunza, kuburudika na kushiriki katika jitihada za vijana wa kitanzania kujenga maisha yao na ya jamii zao.

Huu utakuwa ni msimu wa tatu wa kipindi cha Ruka Juu, baada ya mafanikio ya misimu miwili ya awali ambapo amsimu wa pili ulishindanisha vijana wakulima wajasiriamali.

Msimu huu unawakutanisha vijana sita machachari ambao wanaongeza thamani kwenye mazao ya kilimo.

“Hiii ni Kazi nyingine ya Femina Hip, na kama kawaida ya shirika hili , Kazi zake hufanyika kwa kuzingatia mahitaji ya hadhira yake ikiwa ni mwitikio wa mrejesho unaotoka kwa vijana sambamba na sera na mikakati inayolenga kuwapa vijana hao mbinu za kulinda na kujenga maisha yao,” alisema mmoja kati ya waandaji wa shindano hilo Bahati Mdetele.

Aliongeza, “Tanzania ya sasa ambayo inalenga kujenga uchumi wa viwanja,inahitaji nguvu kazi yenye stadi mahsusi na nia madhubuti ya kuunga mono jitihada hizi. Ruka Juu itatoa mchango katika hili kwa kuwashindanisha vijana hao sita ambas wamethubutu na wameweza. Watatoa uzoefu wao, wataweka bayana changamoto zao, watatushirikisha mbinu zao za kupambana na vikwazo, lakini pia watatupa raha kutokana na jinsi ambavyo watapambana na jumla ya majaribio 10 watayopewa kwenye shindano hilo,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents