Technology

Kiwango cha tarakimu katika ujumbe wa twitter chaongezwa

Mtandao wa kijamii wa Twitter umetangaza jaribio lake la kongeza idadi ya tarakimu za ujumbe ambayo mtu anaweza kuandika kwenye mtandao huo kwa mara moja hadi kufikia 280 ambayo ni mara mbili ya kiwango cha idadi ya tarakimu kilichopo kwa sasa.

Mtandao huu ambao umekuwa na idadi ya zaidi watumiaji milioni mia tatu,umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya ukuaji na hivyo inatafuta namna mbalimbali za kukuza wigo wa watumiaji.

Kundi dogo la watumiaji wa mtandao huo watahusishwa katika jaribio hilo la kuongeza idadi ya maneno ya kuandika.

Kampuni hiyo imesema hiyo ni hatua ya kutatua moja ya changamoto ambayo imekuwa ikiwasumbua watumiaji wengi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents