Habari

Fiesta Dar es Salaam ni Rick Ross ama T.I?

Leo Clouds FM kupitia kipindi cha XXL wanatarajia kumtangaza msanii wa Marekani atakayetua Tanzania kwenye show ya Fiesta ya Dar es Salaam. Tayari majina manne ya wasanii wanaoweza kutua Bongo yameanza kutangazwa ambayo ni Rick Ross, T.I, Snoop Dogg na Drake.

Kituo hicho leo kinaendesha kampeni ya watu kubashiri msanii mmoja atakayetua kwenye Fiesta ambapo watu 200 wa mwanzo watakaopatia watajishindia tiketi za bure kuhudhuria show hiyo.

T.I.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa tuliyoipata kutoka kwa mtu wa ndani wa kituo hicho, Rick Ross ndiye ana nafasi kuwa ya kuja kupiga show kwenye Fiesta ingawa kuna wengine wanaohisi kuwa T,I. ndiye anayeweza kuja. Jibu sahihi litabainika ndani ya saa chache zijazo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents