Muziki

FIFA ya wapunguzia adhabu Blatter, Platini

Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) imetoa uamuzi wa Rais anayemaliza muda wake Joseph Blatter na Rais wa UEFA Michel Platini wamepunguziwa adhabu kutoka miaka 8 hadi 6,Uamuzi huu umetangazwa Jumatano hii na Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA), baada ya wawili hao kukata rufaa.

2D2D7D2200000578-3263820-Blatter_and_UEFA_president_Michel_Platini_left_are_both_facing_s-a-198_1444251713596

Wakati wagombea hao wawili kwenye nafasi ya urais wa FIFA, wakiwa na matumaini kwamba wataibuka washindi.

Kamati hiyo imebaini kwamba wawili hawa wamekutwa na hatia ya kukiuka Ibara nne za maadili ya sheria na wamekutwa hasa na hatia ya mgogoro wa kimaslahi.

Wakati huo huo, Tume hiyo imefutilia mbali madai ya “rushwa” na kufuta rufaa ya kitengo cha uchunguzi cha FIFA ambacho kiliomba Joseph Blatter na Michel Platini wasimamishwe maisha katika shughuli zote zinazohusiana na soka.

Kwa sasa wawili hawa hawana tena matumani ya kufutiwa makosa yanayowakabili, kazi kubwa imebaki kwa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (TAS), ambayo ni Mahakama ya ngazi ya juu katika michezo.

Uamuzi huo mpya wa FIFA ni pigo kubwa kwa Michel Platini, ambae tayari amelazimishwa kuachana kuwania katika kinyan’ganiro cha urais wa FIFA, ambapo alikua amepewa nafasi kubwa ya kumrithi Joseph Blatter.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents