Burudani

Floyd Mayweather amlipa Nicki Minaj tshs mil 81 kuonekana (sio kutumbuiza) kwenye birthday ya mwanae

Si lazima Nicki Minaj aimbe ili aingize mpunga. Kwa mujibu wa vyanzo vilivyouambia mtandao wa TMZ, Floyd Mayweather Jr. amemlipa rapper huyo wa YMCMB, $50,000 (zaidi ya shilingi milioni 81) kuonesha tu sura yake kwenye birthday ya miaka 14 ya binti yake.

10413011_444179745718187_1082321648_n
Nicki na Iyanna

Vyanzo hivyo vimesema Mayweather alikodi uwanja mzima wa MGM huko Las Vegas kusherehekea birthday Iyanna Mayweather weekend iliyopita ambapo Nicki alitokea kumsurprise.

10362086_648769401871575_94349325_n
Mayweather na Nicki Minaj

Nicki alikaa kwa saa moja akipiga picha na Iyanna na kuondoka. Birthday ya Iyanna ndiyo iliyozusha ugomvi wa T.I. na Floyd baada ya mke wake Tiny kupost picha akiwa na Iyanna.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents