Burudani

NSSF: Tumepata wateja wapya 30,000 kutokana na tangazo lililofanywa na Leka Dutigite

Joseph Mbilinyi aka Sugu pamoja na kambi rasmi ya upinzani, inaweza kuwa imekiwekea mchanga kitumbua cha kampuni ya Leka Dutigite, lakini mteja wa kampuni hiyo, ana mtazamo tofauti – in fact ni mteja mwenye furaha.

Kigoma-All-Stars-meeting

Kwa mujibu wa NSSF ambayo iliipa kampuni hiyo takriban shilingi milioni 81 kufanya tangazo na kudhamini show ya Leka Dutigite mkoani Tanga, kampeni ya wasanii hao wa Kigoma imewaongeza wateja wengi.

“Kweli mara ya kwanza tuliwalipa Sh25 milioni wasanii wa kundi hilo ili watutengenezee wimbo na Sh56 milioni zilikuwa za udhamini wa onyesho lao, lakini kwa masharti ya kututangaza jambo ambalo lilikuwa na mafanikio kwetu kwani tumefanikiwa kupata wateja wapya 30,000 kutoka sekta isiyo rasmi,” Meneja Kiongozi wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume amekaririwa akikiambia chombo kimoja cha habari.

Chiume alidai kuwa NSSF ilitumia kiwango hicho cha pesa ili kujitangaza kwa kuwa hata mashirika ya kijamii yanapaswa kufanya hivyo ili kuvutia wateja wengi zaidi.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe jana aliwekwa kwenye kitimoto na Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni, Joseph Mbilinyi aliyemtuhumu kuhusika na kinachoitwa ufisadi katika Shirika la TANAPA na NSSF. Zitto ameamua kujibu tuhuma hizo kupitia Facebook.

Katika hatua nyingine, msanii wa Leka Dutigite, Linex Sunday Mjeda amefunguka na kudai kuwa hajaona mchango wa mbunge Joseph Mbilinyi aka Sugu kwa wasanii wa muziki.

“Hivi toka Sugu amekua mbunge ni kitu gani alishawahi kuwafanyia wasanii wa Taifa hili, Tanzania na akiwa kama waziri kivuli, amewahi kufanya nini kuinua kipato cha wasanii? Je amejenga mazingira gani kuhakikisha wasanii hawawi ombaomba wakutegemea misaada bali wajasiriamali? Eg. Amefikia wapi kwenye suala la hakimiliki na ufuatiliaji wake etc nimeuliza tu manaake kuna vitu vinaendelea sivielewi,” ameandika Linex kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents