Promotion

Fundi viyoyozi atimka na Milioni 20 za Vodacom

Huku siku zikiwa zinahesabika kwa Promosheni ya Timka na Bodaboda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania kufikia ukingoni, Neema imeendelea kuwashukia maelfu ya Watanzania na safari hii ni kwa Willison Urio Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ameibuka Mshindi wa Shilingi Milioni 20.

001 Droo
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akisisitiza jambo wakati wa Droo kubwa ya Mwezi ambapo WillisonUrio (33) Mkazi wa Mbezi Beach Jijini Dar aliibuka Mshindi wa Shilingi Milioni 20. Pamoja nae katika picha ni Ofisa hudum za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambena Ofisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Chiku Saleh. Ili kushiriki katika Promosheni hiyo Mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwendanamba 15544

Promosheni hiyo ambayo imeboresha maisha ya mamia ya Watanzania Tangu kuanza kwake imemuibua mshindi huyo ambae akizungumza kwa njia ya simu wakati alipopigiwa simu akiwa mapumzikoni Mkoani Kilimanjaro alisema kupitia mchezo huo ameona mwanga katika maisha yake kwani alikuwa akijipa matumaini kuwa ipo siku ndoto yake itatimia.

“Maisha ya sasa ni magumu sana na nivigumu kwa mtu wa kawaida kupata kiasi kikubwa cha fedha kwa mkupuo, yaani ni vigumu kuamini kwamba mtu unaweza kupata Milioni 20 kiurahisi tu, lakini leo nimeamini kupitia Vodacom haya yote yanawezekana. Sasa nimeona mwanga katika maisha yangu, nitajiendeleza kibiashara na kuhakikisha ninakuwa na mafanikio na kuendelea kuwaunga mkono Vodacom kwa kuyabadilisha maisha yangu,” alisema Urio.

“Imekuwa vigumu kwangu kuamini kama nimeshinda kiasi hiki cha fedha ninamshukuru sana Mungu, Kuna siku nilisikia mama mmoja kutoka Arusha ameshinda milioni 10, nilikaa siku zote na kujipa matumaini kuwa ipo siku nami nitashinda na sikukata tamaa niliendelea kushiriki katika mchezo huu na leo nimejibiwa maombi yangu na nimeona matunda ya kutokukata tamaa.”

Akizungumzia juu ya promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amesema “mwitikio umekuwa mkubwa sana tangu tunaanza mpaka hapa tulipofikia kwani watu wamekuwa wakijishindia bodaboda kwa ajili ya usafiri ama kuanzisha biashara na pia fedha taslimu ambazo zimekuwa zikitumika kufanyia biashara
na matumizi mengine ya kimaisha.”

“Nia ya Vodacom ni kuhakikisha inaboresha maisha ya wateja wake ambao wamekuwa wakituunga mkono siku zote na kutufanya kuendelea kuwa namba moja, Tunawaahidi tutaendelea kushirikiana nao na kuhakikisha tunaboresha maisha ya wateja wetu kwa kuwaletea promosheni zaidi na zaidi.”

Nkurlu aliongezea kwa kusema “mitaji ni kilio kikubwa cha wajasiriamali wengi nchini. Kuunga mkono jitihada za wajasiriamali nchini kote ni lengo mojawapo la kampuni yetu, hivyo tunaamini kwa bodaboda pamoja na fedha hizi tunazozitoa kwa washindi zitasaidia kupiga hatua kibiashara na kuboresha maisha yao”.

“Ninawasihi wateja wengine wa Vodacom waendelee kushiriki katika Promosheni hii ili nao wapate mafanikio ambayo wengine wameyapata na wanayoendelea kuyapata kwani mwishoni mwa mwezi huu watachezesha droo kubwa ya kupata mshindi wa Milioni 30.”

Hadi kufikia sasa zaidi ya watu 315 wamejishindia pikipiki (bodaboda) huku jumla ya fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 211 zikiwa tayari zimekwisha tolewa kati ya milioni 330. Huku Milioni 119 zikisubiria washindi.
Ili kujiunga na promosheni hii wateja wote wa Vodacom wanatakiwa kutuma neno PROMO kwenda namba 15544.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents