Burudani

G Nako hakunishawishi kufanya ‘Umeme Umerudi’ – ZaiiD

Rapper wa SSK, ZaiiD amesema si kweli kwamba style ya G Nako ya kuimba na kurap katika game ilimshawishi kufanya ngoma yake ‘Umeme Umerudi’.

ZaiiD amesema chimbuko la ngoma hiyo ni kutokana na yeye kusikiliza aina nyingi za miziki tofauti lakini anaheshimu anachofanya G Nako katika game ya Bongo Flava.

“Hapana, mimi pia ni shabiki wa aina nyingi za rap, sijui kwa sababu G Nako naye amefanya, Ngwea alikuwa anaimba na kuchana, Chidi Benz hivyo hivyo, mimi nilikuwa nikisikiza miziki mingi sana” ZaiiD ameiambia Bongo5.

“Namuheshimu G Nako kwa anachofaya ila hakuni-inspire kufanya umeme, niliamua kwa sababu nilihisi ni muda halisi wa kuongea vitu ambavyo vitasika mwanzo hadi mwisho kwa ukaribu na urahisi” ameongeza.

ZaiiD kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Wowowo’ pamoja na ile ya kundi (SSK), Slow Down.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents