Burudani

Godzilla: Tunahudumia kundi kubwa la watu wenye interest zinazotofautiana, huwezi kumridhisha kila mtu

Baada ya Godzilla kuachia wimbo wake mpya, Kila Wakati (Mungu ni Mwema) aliomshirikisha G-Nako, kumekuwepo na mapokeo tofauti.

Baadhi ya watu wanadai kwenye ngoma hiyo wanamsikia Zilla ambaye hawajamzoea. Lakini kwa rapper huyo wa Salasala, mapokeo ya aina hiyo ni kitu anachokitarajia sababu anafahamu kuwa anahudumia kundi kubwa lenye interest zinazopishana.

“Unajua biashara yetu tunadeal na watu wengi so kila mtu na views zake. Unajua kila mtu akikuona wewe, kuna kitu anatarajia kutoka kwako,” Zilla ameiambia Bongo5.

“Unajua ‘too much is given, much is tested’ aliyebarikiwa haachi kujaribiwa, unajua mtu unaimba nyimbo kama ‘waiter leta mitungi’ kuna mlevi alishazoea party anataka upige kama ile. Halafu unapiga labda ‘Mungu ni mwema’ kuna mtu wa gospel kesho anataka utoe kama hii. Kwahiyo unatoa huduma kwa watu wengi ambao kila mtu anataka kukusikia kwa angle yake aliyowahi kukusikia, it’s impossible,” amesisitiza.

Zilla amedai kuwa kwa kuzingatia hivyo, inabidi ahudumie kila interest za watu mbalimbali kupitia nyimbo zake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents