Burudani

Haikuwa rahisi kuhitimu IFM – Ayler (Audio)

Si wasanii wote waliosoma kwenye chuo cha usimamizi wa fedha, IFM walimaliza kozi zao.

13269593_272006773148785_739600591_n

Wengi waliishia njiani kutokana na jinsi chuo hicho kilivyo strict huku wasanii wenye ratiba nyingi za show wakishindwa kufua dafu. Lakini si kwa muimbaji wa ‘Nenda’, Ayler.

Ayler amesema kwenye kipindi cha Chill na Sky kuwa baadhi ya wahadhiri wa chuo hicho wamekuwa na kasumba ya kuwakomalia wasanii wanaosoma hapo wakiamini kuwa wasanii ni watu wa kula bata tu.

“Sometimes walimu wanakutengenezea vikwazo tu upate tu sup uende ukajibebishe lakini no way out I was really studying hard ukikutana na watu nimesoma nao watakumbia kwamba mimi I work so hard. I was really working hard.”

Amesema hadi alipohitimu chuo alimshukuru Mungu. Ayler alihitimu shahada ya Computer Science. Wasanii wengine waliowahi kusoma chuo hicho na kushindwa kumaliza ni Ben Pol, M-Rap na wengine.

Msikilize Ayler hapo chini kwenye Chill na Sky.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents