Tazama picha za Halloween za mastaa wa Marekani, zifahamu pia sherehe hizo zina maana gani
Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa Instagram, bila shaka siku za hivi karibuni hasa Jumapili na Jumatatu hii umekuwa ukiona picha za mastaa kibao wa Marekani wakiwa wamevaa nguo za ajabu ajabu na kuandika #Happy Halloween!
Alicia, Swizz Beatz na familia yao
Tunaamini umeona pia baadhi ya watanzania wakiwa wamevaa nguo za aina hiyo na kuandika kitu hicho hicho. Lakini bado ukweli ni kuwa watu wengi sana duniani hawafahamu maana na chimbuko la sikukuu hii.
Chris Brown
Tinashe
Halloween ni miongoni mwa sikukuu kongwe zinazoendelea kusherehekewa hadi leo hii. Ni miongoni mwa sikukuu maarufu duniani, pengine ya pili baada ya Christmas.
Jay Z na Beyonce
Wakati mamilioni ya watu wanasherehekea Halloween bila kujua chimbuko lake, historia na ukweli wake, hufanya sikukuu hiyo ivutie zaidi. Baadhi ya watu huichukulia Halloween kama muda wa kufurahi, kuvaa nguo tofauti na kula bata kwa party za aina mbalimbali.
August Alsina
Wengine huiona kama muda wa masuala ya kishirikina, mizimu, mahoka na uchawi mwingine ambao unapaswa kuepukwa kwa gharama yoyote. Halloween pia ni sikukuu ambazo kwa dini kama ya kikristu zimeleta mkanganyiko kwa muda mrefu.
Fergie na Josh Duhamel
Historia ya Halloween
Nicki Minaj
Halloween hufanyika kila October 31, siku ya mwisho ya kalenda ya Celtic. Awali siku hiyo ilikuwa ni siku ya wapagani kuwakumbuka waliokufa. Halloween ilikuwa ikimaanisha ‘All Hallows Eve’ na hiyo ni zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Ariana Grande
All Hallows Eve hufanyika jioni kabla ya All Saints Day, iliyotengenezwa na Wakristo kuwabadilisha wapagani na husherehekewa November 1. Kanisa katoliki huwaenzi watakatifu wake katika siku hii.
Kelly Rowland
Chimbuko la Halloween
Pamoja na kuwa na aina nyingi za machimbuko na mila za zamani, mengine yameendelea kubakia vilevile. Tamaduni tofauti huchukulia Halloween kwa aina tofauti lakini mila za Halloween zimebaki kuwa zilezile.
Iggy Azalea
Utamaduni wa Halloween unakumbukwa enzi za Druids, utamaduni wa Celtic huko Ireland, Uingereza na Ulaya Kaskazini. Kulifanyika karamu ya Samhain, iliyokuwa kila mwkaa October 31 kuwakumbuka waliokufa. Samhain inamaanisha “summers end” yaani mwisho wa kiangazi au November.
Karrueche Tran
Samhain ilikuwa ni sherehe ya mavuno na uchomaji wa moto kumaliza mwaka wa Celtic na kuanza mpya. Mambo mengi yaliyokuwa yakifanyika kwenye sherehe hizo yalihusiana na imani za kishirikina.
Jhene Aiko
Celts waliamini kuwa nafsi za waliokufa zilikuwa zikizunguka mitaani na vijijini usiku. Kwakuwa si mizimu yote ilikuwa ikiaminika kuwa salama, zawadi mbalimbali zilikuwa zikiweka nje kuituliza ile mibaya kuhakikisha mavuno ya msimu ujao yatakuwa mazuri.
Jojo
Mila hiyo huhusisha trick-or-treating ambapo watoto huzunguka nyumba hadi nyumba kuomba kupewa vitu mbalimbali kama chakula nk.
The Game
Rihanna
Usher
Ludacris na mke wake Eudoxie