Habari

Halotel yatoa Msaada kwa Wanawake Wenye Mahitaji Maalumu Mtwara

Halotel wakikabidhi msaada wa Vifaa vya nyumbani na Chakula katika taasisi ya Jukwaa la Wanawake walemavu Mtwara. Kushoto akiwa Mkurugenzi wa Tawi la Halotel Mtwara Bw. Emmanuel Monyo, Kati ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Jukwaa la Wanawake walemavu Mtwara Bi. Fatuma Mohamed Mkondomoka, Kulia Afisa uhusiano na Mawasiliano makao makuu Halotel Bi. Roxana Kadio.

Katika kuhadhimisha mwezi wa kumsheherekeaMwanamke na kukaribisha sikuukuu za Pasaka, Halotel Tanzania yatoa msaada kwa wanawake chini ya Taasisi ya ‘Jukwaa la wanawake na wasichana wenye ulemavu Mtwara’ kusaidia changamoto mbalimbali wanazozipata wanawkae hao.

 

Halotel ikiwa ni kampuni ya mawasiliano Tanzania, ikitoa huduma mbalimbali za mawasiliano na ikiendelea kukidhi mahitaji ya wateja wao. Kwa kuzingatia usalama na uaminifu Halotel inaendeleakutoa huduma bora na kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya mawasiliano na jamii kiujumla.

Akiongea katika tukio hilo Mkurugenzi wa Halotel tawi la Mtwara Bwana Emmanuel Monyo “Halotel inaendelea kusimama imara katika kufanikishamalengo yake ya kukuza usawa na ujumuishaji katika pande zote za jamii. Lakini kwa kuwasaidia wanawakehawa Mtwara Halotel inaonyesha dhamira yake ya kuleta mabadiliko katika jamii na kuunda ulimwengu weye uwezekano na fursa kwa wote”.

Afisa uhusiano na mawasiliano wa Halotel, Roxana Kadio ambae aliwasilisha msaada huo alisema Halotel inaedelea kujenga ujumuishaji ambao kila mtu bila kujali uwezo wao anaweza kushiriki kikamilifu katika jamii, aliendelea kusema kuwa Halotel iliamuakuwasupot wanawake wa Mtwara baada ya kujifunza kuwa wanapitia changamoto za chakula na vifaa vya nyumbani na kama kampuni inayokua nia yetu kutoa mkono wa msaada kwa jamii ya kitanzania.

Mahitaji yaliyotolewa na Halotel ni pamoja na Chakula kama Mchele, Sukari na Mafuta ya kupikialakini pia kutoa msaada wa magodoro na vifaa vinginevya nyumbani. Vyote hivi ni katika kuwahudumiawanawake hawa na kuwaonesha kuwa hawako pekeyao katika changamoto wanazozipita” Roxana alisema. Aliendelea kusema kuwa msaada huu pia unalengakatika kuwatoa upweke wanawake hawa katika mahitaji yao. Na kwamba Halotel haitoishia kusaidia tu wanawake na wako kwenye mpango wa kukuza uhitajiwa jamii kiujumla.

Halotel itaendelea kutoa ushirikiano kwa majukwaaambayo yanajikita katika kuwainua wanawake. Lakinipia Halotel itaendelea kutia chachu ya maendeleo kwa wateja wake na jamii kiujumla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents