Habari

Moto wa mkaa waua Mtoto

Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi nane, Iyan Kingao, Mkazi wa Mtaa wa Igangidung’u Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe amefariki baada ya kuungua moto uliotokana na jiko la mkaa huku Mama yake akiwa ametoka kwenda kupokea mafuta ya kupikia barabarani kwa Dereva wa pikipiki. Mama wa Mtoto huyo, Anna Mabiki (28) amesema alimwacha Mtoto wake ndani majira ya saa mbili usiku akiwa amelala kwenye kochi na kwenda kupokea mafuta na aliporudi alikuta tatizo hilo la moto “Nageuka nyumbani nakuta kuna moto tukaanza kukimbia na yule Kaka, kuja kumuokoa Mwanangu nikakuta nguo zimeshika moto na kumshika mkono nimuokoe bahati mbaya akateleza na kuanguka Watu wakasema subiri tumtoe wenyewe wakanitoa nje” Mwenyekiti wa Mtaa wa Igangidung’u Emmanuel Gadau na Afisa Mtendaji wa Mtaa huo Happness Sanga wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo wamesema licha ya Mtoto huyo kupoteza maisha pia TV pamoja na kochi vimeteketea kwa moto na kuwataka Wazazi kuwa karibu na Watoto mara kwa mara.

Kwa upande wake Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kipolisi Makambako Gotfrid Kimboy akiwa eneo la tukio amewataka Wananchi kuacha tabia ya kulala na majiko ya mkaa ndani “Ukiachia mbali moto ulishika kochi na kuunguza alipokuwepo Mtoto lakini ni lazima tuwe makini na haya majiko tunavyoweka ndani”

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents