Burudani

‘Hasara Roho’ ya Darassa ni noma!

Huenda rapa Darassa kupitia wimbo wake mpya ‘Hasara Roho’ akavunja baadhi ya rekodi alizoziweka mwaka 2016 kupitia wimbo wake uliopita ‘Muziki’.

Darassa

Video ya wimbo huo aliyoiachia May 5 mwaka huu kupitia mitandao wa YouTube tayari imeangaliwa mara 933,776 ndani ya siku 12 kitu ambacho siyo cha kawaida.

Rapa huyo kupitia video ya wimbo wake ‘Muziki’ aliweka rekodi mbalimbali ikiwemo ya video hiyo kuangaliwa mara elfu 71 ndani ya saa 24.

Video ya Muziki mpaka sasa kupitia mtandao wa YouTube imeangaliwa mara 7,859,849 kwa kipindi cha miezi mitano.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki katika mitandao ya kijamii wanadai ‘Hasara Roho’ haiwezi kuvunja rekodi mbalimbali zilizowekwa na wimbo ‘Muziki’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents