Burudani

Hata nikifa leo huwenda nisiache pengo – Fid Q

Msanii wa muziki wa hip hop, kutoka mkoani Mwanza, Fid Q amedai kwa vipaji alivyoviona mkoani humo hata akifa leo hawezi kuacha pengo lolote kwenye muziki huo.

Rapa huyo alitoa kauli hiyo mapema wiki hii mkoani Mwanza akiwa katika Tamasha la Sport & Music Festival baada ya kuona kipaji cha kijana mdogo aitwae, Aga Star.

Kijana huyo alipanda jukwaani na kuanza kuchana hali ambayo ilimfanya Fid Q kumpatia nafasi zaidi kutokana na uwezo ambao aliuonyesha.

“Unajua kuna wakati tunafikiria vitu vingi kwenye huu muziki, lakini nilichogundua leo hata nikifa leo huwenda nisiache pengo kama kuna vijana kama hawa ambao wanaonyesha uwezo mkubwa katika uandishi na kuchana,” alisema Fid Q.

Aga Star baada ya kuonyesha uwezo mkubwa alipatiwa ofa ya kurekodi wimbo chini ya producer Mr Ttouch huku DJ Tass akiahidi kumsaidia kwenye promotion.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents