Michezo

Mchezaji wa Denmark akodi ndege binafsi kukiwahi kichanga nyumbani

Beki wa timu ya taifa ya Denmark ambayo ipo kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Urusi, Jonas Knudsen amejikuta akikodi ndege binafsi na kurejea nyumbani kwao ili kumuona mtoto wake mchanga ambaye amezaliwa kabla ya muda wake.

Mara baada ya ushindi wa timu ya taifa ya Denmark dhidi ya Peru mchezo wa kundi C uliyopigwa Juni 16 nchini Urusi, Knudsen alipata ujumbe unaomueleza kuwa mkewe, Trine amejifungua mtoto wa kike wiki chache kabla ya muda wake habari zilizomshtua  mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 na kuamua kurejea kwao.

Baada ya tukio hilo mlindalango wa timu ya taifa ya Denmark Kasper Schmeichel amesema kuwa licha ya kuwa wao ni wachezaji lakini wasisahaulike kuwa nao ni binadam.

“Nafikiri nilazima tukumbuke kuwa nasi ni binadam licha ya kuwa ni wachezaji, nikiwa kama baba najiuliza Jonas ni hali gani anapitia kwa sasa hasa mara baada ya kupata ujumbe huu ilihali hayupo nyumbani,” Kasper Schmeichel.

“Tupo wazazi wengi ndani ya kikosi chetu kwa hiyo tunapaswa kulichukulia swala hili kiubinadam na kufanya kilakitu kuweza kumsaidia kumuona mwanae.”

Knudsen amerejea kwenyetimu yake ya Denmark  siku ya Jumatatu ya wiki hii tayari kujiandaa na mchezo wao wa kundi C dhidi ya Australia utakao pigwa leo siku ya Alhamisi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents