Burudani

Hatufanyi muziki kwa kujifurahisha – Mwana FA

Msanii wa Bongo Fleva, Mwana FA amesema kutokana na soko la albamu Bongo kuanguka ndio imepelekea wasanii wengi kutokutoa albamu kwani biashara hamna.

Rapper huyo ameeleza kutoa albamu wakati hamna biashara ni vigumu ingawa hicho ni kipimo cha wasanii kukua.

“Hatufanyi muziki kwa sababu ya kujifurahisha, kama haileti pesa inakua ngumu kufanyika, so nafikiri kuwepo na namna ya kutumia hizi teknolojia tulizonazo kuhakikisha albamu zinauzika,” Mwana FA amekiambia kipindi cha XXlL cha Clouds FM.

“Hivi vitu vilikuwa vinafanyika miaka kadhaa iliyopita na mimi ninavyoona msanii hawaulizwi una nyimbo ngapi, haijawahi kutokea hiyo, muziki wako unatambulika kwa kufahamika msani huyo ana albamu ngapi. Kidogo naona angalau mwaka huu wasanii wawili watatu kama Navy Kenzo wametoa albamu na wengine wanatengeneza albamu zao ni dalili nzuri,” ameongeza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents