Habari
Hawa ndio madereva 10 waliofungiwa na Waziri Simbachawene leo (+ Video)
Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mhe George Simbachawene amewafungia kwa muda wa miezi mitatu Madereva 10 wa Mabasi ambao wamekuwa wakikiuka Sheria ya usalama Barabarani kwa kuendesha vibaya magari ya abiria.
Waliofungiwa ni Madereva wa Mabasi ya Kampuni za Kimotco (Arusha- Musoma), Al Saedy (DSM- Kilombero), MB Coach (DSM – Arusha), Baraka Classic (DSM – Masasi), Maning Nice (DSM – Tunduma), Machinga (DSM-Mtwara), Ester Luxury (DSM- Moshi), NBC Classic (Tabora – Kigoma), Kilimanjaro Express (DSM- Arusha) na Kapricon (DSM – Moshi)