Burudani

Hawa ndio mastaa 2 ambao Dayna Nyange anatamani kufanya nao kazi

Dayna Nyange amewataja mastaa wa Afrika ambao anatamani kaufanya nao kazi.

Hitmaker huyo wa Komela, amemtaja Wizkid na Patoranking (wote kutoka Nigeria) kuwa ndio wasanii anawapenda na anawafuatilia hivyo anatamani kufanya nao kazi japo wapo wasanii wengi ambao anatamani kufanya nao.

“Nampenda Wizkid ni mtu ambaye ninamuangalia kazi zake, Patoranking pia napenda kazi zake japo wapo wengi ambao natamani kufanya nao kazi,” Dayna ameiambia Bongo5.

Wakati huo huo Dayna ambaye hajawahi kufanya kolabo na msanii mwengine wa kike ameongeza kuwa kuna muda anafikiria kufanya nao kazi lakini pia inategemea na idea ya wimbo wake japo ameahidi kufanya hivyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents