Burudani

Hii ni sababu kwanini Shah Rukh Khan hana mpango wa kwenda Hollywood

Katika muda ambao waigizaji wengi wa India kwa sasa wameelekeza macho yao Hollywood, superstar Shah Rukh Khan ana mtazamo tofauti.

Yeye anadai kuwa ataendelea kufanya filamu India hadi pale atakapotengeneza filamu ambayo dunia nzima itaipenda. “Ndoto yangu siku zote imekuwa ni ndogo na ndoto yangu ni kutengeneza filamu moja India ambayo dunia nzima itaipendda na kuwa kubwa India. Kama nikiifanya kama mtayarishaji, muigizaji, mtu wa taa, au mtu wa kamera, vyovyote vile, nataka tu kutengeneza filamu hiyo moja hapa India,” SRK alisema kwenye mahojiano.

Alipoulizwa kuhusu Priyanka Chopra na Deepika Padukone ambao tayari wameingia Hollywood, muigizaji huyo mwenye miaka 51 alisema, “ni shukrani nyingi kwa Deepika na Priyanka, nadhani kwa walichokifanya ni chachu kwa waigizaji wengi pia kwenda Hollywood.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents