Michezo

Hii ni vita: Klabu tano Premier League zapambana kuwania saini ya Philippe Coutinho

Klabu tano kutoka Premier League zipo katika vita kubwa ya kuwania saini ya mchezaji wa Barcelona, Philippe Coutinho katika msimu huu wa majira ya joto na hii ni kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania.

Mundo Deportivo has claimed five Premier League clubs want to sign Philippe Coutinho

Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool ambaye kwa sasa anaitumikia Bayern Munich inayoshiriki ligi ya Bundesliga kwa mkopo ameanza kuwa lulu kwa klabu hizo za Uingereza.

Barcelona haina mpango tena na Coutinho baada ya kushindwa kufanya makubwa kama yalivyotarajiwa na miamba hiyo ya soka kutoka LaLiga baada ya kujiunga akitokea Anfield mwezi Januari mwaka 2018.

Akiwa katika ukurasa wa mbele wa Deportivo hukukiwa na kichwa cha habari kikubwa kilichoandikwa ‘Premier Coutinho’. Chelsea, Newcastle, Manchester United, Arsenal na Leicester zote zimeonyesha nia ya kutaka huduma ya Mbrazil huyo lakini klabu zote hizo zinadaiwa kutaka kutoa kitita cha paundi milioni 90 ili kukamilisha dili hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents