Michezo

Hili linalotokea kwenye tasnia ya ngumi Tanzania nani wa kulaumiwa?

Floyd Mayweather ni miongoni mwa wanamichezo matajiri duniani. Amefanikiwa kupambana mapambano 49 na kufanikiwa kushinda yote.

DSC_0588

Miaka ya nyuma Tanzania ilionekana kufanya vizuri kwenye mashindano ya ngumi ya kimataifa. Kila mtu aliogopa kupangiwa pambano na Rashid Matumla wa kipindi kile, umaarufu aliokuwa nao ni tofauti na maisha yake anayoishi kwa sasa.

Siku ya Pasaka yalifanyika mapambano kadhaa ya ngumi ndani ya uwanja wa taifa, Mada Maugo dhidi ya Dullah Mbabe, Mohamedi Matumla na Cosmas Cheka, Fransis Miyeyusho na Nasibu Ramadhani.

Pambano hili lilikuwa na lawama nyingi kuanzia kwa mashabiki mpaka mabondia wenyewe. Ubovu wa ulingo ilikuwa ni moja kati ya changamoto zilizokuwepo, sina uhakika na upande wa maamuzi majaji waliamua ya kwao japo baadhi ya mabondia hawakukubaliana na matokeo hayo.

Mada Maugo aliiambia Bongo5, “Tangu nianze kucheza ngumi Tanzania na nje sijawahi kukutana na ulingo mbovu na unashake kama ule. Siyo kwenye pambano letu tu hata kwenye mapambano mengine yaliyofanyika.”

Mmoja kati ya wadau wakubwa wa michezo, Kassim Lyogope alisema, “kutokana na madudu yanayoendelea kwenye tasnia ya ngumi hapa nchini, ndiyo maana tunashindwa kufanya vizuri mabondia wetu wanapoenda nje kupambana na mabondia wa kigeni. Viongozi wa ngumi na mapromota huwaandaa mabondia wao kwa kuwapa matokeo ya kuwabeba wanapo pambana.”

TPBC na TPBC kila siku vimeendelea kunyoosheana vidole kwa kila chama kumtuhumu mwenzake ndiyo mchawi. Tanzania imeshindwa kupeleka timu ya ngumi kwenye mashindano ya Olimpiki yatakayo fanuika nchini Brazil kwa madai ya ukata.

‘Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni’, sitamani kuona kinachotokea kwenye michezo Tanzania bora miaka irudi nyuma tumuone Matumla alivyokuwa anapambana kwenye ardhi ya Marekani na kupata ushindi. Sitamani kuona kilichomtokea Thomas Mashali wiki kadhaa zilizopita ndani ya ardhi ya Norway kwa kulambishwa sakafu kwa kipigo.

Lakini pia Rais wa TPBO, Yasini Abdallah Ostadh amesema, “Bado Tanzania hatujapata ulingo uliokuwa mzuri wa kupambania. Wachezaji wengi wa ngumi wanakosa nidhamu ndiyo maana wanaonekana kutofanya vizuri. Kuna watu wengi wapo nje wanaongea kuhusu ngumi, wanatakiwa kama kweli wanaweza wagombee nafasi za uongozi ili kusaidia tasnia ya ngumi isipotee.”

Japo yupo Fransis Cheka anatubeba, lakini nakumbuka kuwa umri hauna hodi. Nani wa kututoa huku tulipo na kutupeleka kule walipo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents