Burudani

Hili ndilo jina la album ya Hemedy PhD itakayotoka Feb mwishoni

Hemedy PhD amesema hatimaye mwezi huu atatimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kuachia album yake.

20160201184705

Muimbaji na muigizaji huyo wa filamu ameiambia Bongo5 kuwa album yake iitwayo Virgo itatoka mwezi huu.

20160201184743

Ijumaa hii amesema ataachia wimbo uitwao ‘Where You Are’ aliomshirikisha Gelly wa Rhymes na Gosby utakaokuwemo kwenye album hiyo. Wimbo huo umetayarishwa katika studio za Sei Records.

Album yangu Virgo itakuwa na ngoma 12 na hiyo ikiwemo. Itakuwa out mwezi wa pili mwishoni na kuna collabo kali mbili zinafuata before album kutoka. Mashabiki zangu wakae mkao wa kula,” amesema Hemedy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents