Burudani

Hisia aileta ‘Muziki wa Hisia’ Dar, Grace Matata, Damian, Heri Muziki kumsindikiza Jumamosi hii

Muimbaji wa muziki wa soul, Hisia ameileta show yake ya muziki wa live iliyokuwa ikifanyika jijini Arusha, Dar es Salaam.

Show hiyo itafanyika Jumamosi ya May 16 kwenye ukumbi wa Thai Village.

Akiongea na Bongo5, Hisia amesema kwenye show hiyo ya kwanza kuwahi kufanyika Dar es Salaam, Grace Matata, Damian Soul, Heri Muziki na wengine watamsindikiza.

Pia mchekeshaji MC Pili Pili atakuwepo kuzivunja mbavu za watu watakaohudhuria show hiyo.

“Ni kitu fulani tulianzisha Arusha, it’s a live music platform, ni platform ya kutangaza muziki wa live na pia muziki wenye ladha tofauti kidogo na kinachosikika zaidi redioni na kwenye TV,” Hisia ameiambia Bongo5.

“Utakuta kuna jazz, afro-fusion, afro-soul, kuna reggae pia hapo, tunapromote hip hop lakini watu wanaofanya hip hop live kama Fid Q siku hizi anafanya sana.”

Mtazame zaidi hapo juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents