Burudani

Hizi taarifa nazichukulia tu kama uvumi naamini BASATA hawawezi kunifungia wimbo – Roma

Licha ya BASATA kutoa maelezo ya jinsi ambavyo wanaweza kuufungia wimbo wa msanii kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari pasipo kumwandikia msanii barua yoyote (Ingia hapa), Roma bado anaamini kuwa Baraza hilo la sanaa halijaufungia wimbo wake.

viva roma

Akizungumza kupitia Planet Bongo ya EA Radio, Roma amesema kuwa anaamini BASATA wanasapoti kazi zake hivyo taarifa za kuufungia wimbo wake anazichukulia kama uvumi tu.

“BASATA wanasapoti kazi za wasanii, kwa hiyo huwezi kuniambia kwamba wimbo wa Roma umefungiwa, BASATA hawawezi kutoa maamuzi kama hayo ya kufungia ngoma ya Roma, me i’m sure BASATA wanasapoti kazi ya sanaa na wanamsapoti Roma, na hizi taarifa nazichukulia tu kama rumors,” alisema Roma.

Rapper huyo ambaye amekuwa kwenye headlines toka aachie wimbo mpya wa Viva Roma Viva (VRV) ameendelea kusisitiza kuwa kinachomfanya aamini kuwa hajafungiwa ni kwasababu hajapokea barua yoyote kutoka BASATA.

“Kwanza hakuna Officia letter ambayo nimepewa, pili nikiangalia mifano kama ambayo nimekupa na vyenye ambavyo wao wamesema kwa mtazamo wao, hapana kwa chombo kama BASATA hawawezi kuangalia kwa jicho hilo, mi nawaamini BASATA na najua kabisa lazima wasapoti kazi zangu.” Alisema Roma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents