Burudani

Huddah Monroe amkana Colonel Mustafa, adai alitafuta ‘kiki’ kupitia jina lake

Mwezi uliopita aliyekuwa mwakilishi wa Kenya kwenye BBA, Huddah Monroe na Colonel Mustafa walitangaza uhusiano wao wa kimapenzi kwenye kipindi cha ‘Kiti Moto’cha KTN.

Bgaa6uhIgAA4Drv1

Hata hivyo, Huddah ameibuka na kusema interview hiyo ilikuwa imepangwa. Kwenye interview hiyo, wawili hao walidai kuwa wanapendena na wanaweza kufunga ndoa. Hata hivyo kwenye mahojiano na mtandao wa Ghafla, Huddah amekanisha kuwa na uhusiano na rapper huyo.

Amesema Ogopa Dj na Mustafa ni meli inayozama na hivyo walihitaji kupata boost kutoka kwake.

“Simjui Mustafa, sijui anapoishi. Siku ya kwanza tumekutana ilikuwa kwenye upigaji picha na tulienda kwenye interview na KTN. Nataka kueleweka kuwa Mustafa sio class yangu, sio wa kiwango changu na kila mmoja anajua siwezi kuwa na uhusiano naye ukiachilia mbali mashabiki wake 300.

Katika hatua nyingine, Huddah amejiondoa kwa muda kwenye mtandao wa Twitter.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents