Burudani

D-Knob: ‘Stress nilizielekeza chuo’ asema wasanii wapya ni waandishi wazuri kuliko wa zamani

Rapper Innocent Sahani aka D-Knob, amesema wakati ambapo baadhi ya wasanii walijikuta wakiamua kupunguza stress za maisha kwa kujiingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya, yeye alielekeza stress zake katika kusoma kwa bidii.

VHVkbTBw

Akiongea kwenye kipindi cha Mkasi cha jana, D-Knob alisema ilifika wakati alijikuta akiwa na maisha magumu na kujikuta akikosa hata buku mfukoni. “Mimi nimewahi kuwa hivyo, halafu sasa sina hela unajua mimi nilishazoea, nilipotoa ile Elimu ya Mtaa na Sauti ya Gharama, niilishazoea kila siku sikosi kuwa na laki mbili, laki tatu na shule yenyewe nikaacha nikaona nimeshawin maisha, unajua zile halafu ikafika kipindi hata buku huna,”alisema D-Knob ambaye amerejea tena kwenye chart na wimbo wake ‘Nishike Mkono’ aliomshirikisha Mwasiti.

“Kipindi hicho nikawa na mastress mengi ndio kipindi ambacho nilienda shule,” alisema. D-Knob alisema alipojiunga chuo alikuta watu wameshaanza kusoma na ilipita zaidi ya miezi sita kabla ya familia yake kujua kuwa anasoma.

“Stress zangu mimi nilizielekeza chuo. Mimi ndio maana nawaambia watu, sihitaji kuona miujiza ya shehe au padre anamuombea mtu mpaka anasimama ndio niamini kwamba kuna maajabu duniani. Nikiangalia tu mimi nilivyopita maisha yangu ni miracle tosha.”

Katika hatua nyingine D-Knob alisema wasanii wa sasa hivi wanajitahidi zaidi kuandika ukilinganisha na wale wa zamani.

“Watu wa sasa hivi unaweza ukawasikiliza ukaenjoy yaani. Watu wanaoimba, Diamond anaandika vizuri sana. Watu wa hip hop karibia wote ni waandishi wazuri navutiwa kuwasikiliza.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents