Habari

Hussein Machozi aeleza changamoto aliyopata kubadilisha wimbo wake ‘Mdogo Mdogo’ kuwa ‘Ulikuwa Wapi’ (Video)

Kabla ya Diamond hajatoa wimbo wake ‘Mdogo Mdogo’, Hussein Machozi alikuwa na wimbo wenye jina hilo.

Hata hivyo hakupenda kuendelea kutoa wimbo huo kwa jina hilo kwakuwa hakutaka watu wadhani kuwa amekopi wazo la msanii mwenzake japo anakiri hicho hakikuwa kitu rahisi.

“Ilinibidi kwasababu sikutaka kufanana,” Machozi aliiambia Bongo5.

“Unajua raia pia hawatabirikagi, wanaweza wakasema jamaa kakopi. Basi nikaona tu tukae tubadilishe na watu wangu wa karibu.”

Hussein anasema alikishirikisha kituo cha redio cha RFA kupitia wasikilizaji wake kupata jina jipya.

Wimbo huo sasa umetoka ukiwa video yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents