Technology

Infinix HOT 10 Play kuja kuwanufaisha wafanyabiashara wa mtandaoni

Kama kuna simu unafikiria kununua kwa sasa basi ningekushauri uwe na subira kidogo kwani muendelezo wa series ya HOT 10 yenye kufahamika kama HOT 10 play mbioni kuingia sokoni wakati wowote kuanzia sasa.

Tovuti mbalimbali zimekuwa zikisifu ubora uliopo katika simu hiyo mpya iliyozinduliwa nchi za jirani kama vile Nigeria. Infinix HOT 10play inasemekana moja ya sifa zake ni namna ilivyo na uwezo wa kupiga music bila wa uhitaji wa sub-woofer kukongo nyoyo zako na hii ni kutokana na namna teknlojia ya DTS Audio ilivyo imarishwa zaidi.

Infinix HOT 10play inasemekana kuwa simu ya kwanza katika series ya HOT 10 ambayo warembo/fashionista wataifurahiya sana ni simu yenye resolution kubwa yenye kuongeza ubora wa pixel za kamera ya HOT 10play na tutegemee kuona maajabu ya MP 8 za kamera ya mbele na MP 13 za Kamera ya nyuma.

Tembelea https://www.infinixmobility.com/tz/ ili kufahamu zaidi kuhusiana na bidhaa zao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents