Habari

Iran, China na Urusi zafanya mazoezi ya kijeshi pamoja baharini

Iran, China na Urusi zimefanya luteka za kijeshi za pamoja katika eneo la Kaskazini mwa bahari ya Hindi hii leo.Haya yameripotiwa na shirika la habari la serikali ya Iran.

Russia, China, Iran to Hold Joint Naval Drills on Friday - The Moscow Times

Msemaji wa zoezi hilo Mostafa Tajoldini amesema kuwa vikosi vya jeshi la serikali na kikosi maalumu cha nchi hiyo cha walinzi wa mapinduzi vinashiriki katika zoezi hilo la ukanda wa usalama wa baharini wa 2022.

Taljodini ameongeza kuwa madhumuni ya zoezi hilo ni kuimarisha ulinzi na usalama na misingi yake katika kanda hiyo pamoja na kupanua kimataifa ushirikiano kati ya mataifa hayo matatu kwa pamoja kusaidia katika amani duniani na usalama wa baharini kwa maslahi ya pamoja ya baadaye.

Taljodini pia amesema kuwa luteka hizo zitajumuisha mazoezi kadhaa kama vile kuokoa meli inayoteketea, kuokoa meli iliyotekwa nyara, na kupiga risasi kwenye shabaha za angani usiku.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents